×

Tamko la Serikal Kuhusu Madereva 24 Waliotekwa Kongo na Kikundi cha Mai-Mai

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga akisoma taarifa yake.

 

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema imefanya jitihada za kuwaokoa madereva 24 waliotekwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) na kikundi cha waasi cha Mai-Mai kilichowateka Juni 29 mwaka huu.

 

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga amesema kuwa Kati ya madereva hao 24 waliotekwa 21 ni Watanzania na watatu (3) ni Wakenya na malori 21 yaliyotekwa 19 ni ya Kampuni ya Alistair na mengine mawili ni ya Kampuni ya Primefuels zote za Tanzania.

 

“Tukio hilo lilitokea katika eneo la Lulimba takribani kilometa 100 kutoka mji wa Baraka jimbo la Kivu Kusini, madereva hao walikuwa wanaelekea kwenye mgodi wa dhahabu wa Namoya uliopo jimbo la Mainiema unaomilikiwa na Kampuni ya Banro Gold ya Canada,amesema Kasiga.

 

 

“Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ubalozi wa Tanzania Nchini DRC, waasi wa Mai-Mai walishambulia msafara Wa malori hayo uliokuwa unasindikizwa na askari wa jeshi la DRC (FARDC) na kufanikiwa kupora mali zao zote zikiwemo fedha na kuharibu baadhi ya malori kwa kutoboa matairi na kuvunja vioo.

 

Ameeleza kuwa hadi sasa baadhi ya hatua ambazo serikali kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini DRC imezichukua ni pamoja na kuwasilisha rasmi tukio hilo kwa serikali ya DRC na kuiomba isaidie kuwaondoa watanzania hao katika eneo hilo hatari kwa usalama wao.”

Aidha tumesisitiza kuwa oparesheni inayoendelea ya FARDC dhidi ya waasi wa Mai-Mai itambue uwepo wa madereva hao na umuhimu wao kuwaokoa,”alisema Kasiga.

 

PICHA NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

Leave a Comment