
KWA msimu huu wa maonyesho ya Sabasaba, kampuni maarufu ya simu za mkononi nchini Tanzania, Tecno, inazidi kuendelea kuwajali wateja wake bila ya kujali vipato vyao.

Tecno imetambulisha sokoni simu mpya maarufu kama TECNO DUDE, simu hiyo imekuja kama mkombozi kwa Watanzania wenye kipato cha chini waliokuwa hawana uwezo wa kumiliki simu zenye teknolojia ya kisasa ya kimtandao na zenye kasi ta 4G (fourth generation).

Tecno imekuletea simu hiyo ambayo utaipata kwa Sh 180,000. Simu hiyo ambayo mbali na kupatikana madukani mbalimbali hapa nchini, pia ukifika kwenye Viwanja vya SabaSaba inapatikana.
Mwandishi Wetu