
KAMPUNI ya Wanene Entertainment yenye maskani yake Mikocheni jijini Dar leo imesaini makubaliano na Zanzibar International Film Festival (Ziff) kwa ajili ya kukuza sanaa ya Afrika Mashariki kupitia kipengele kipya cha Tamasha la Ziff cha Trace Best East African Video Music Award mwaka 2017.
Wanene wamejitolea kudhamini kwa kurekodi bure video ya mshindi wa kipengele hicho cha Trace Video Bora ya Msanii wa Afrika Mashariki kupitia Tamasha la Ziff la mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Masoko wa Ziff, Ishaka Mlawa amesema kuwa wameamua kuanzisha kipengele hicho kwa ajili ya kuhakikisha wanachangia kuipeleka mbele sanaa ya Kiafrika.
“Tumeanzisha kipengele kipya ambacho kitatoa nafasi kwa wasanii wa Afrika Mashariki kushiriki na mshindi wa Kipengele cha Video Bora ya Afrika Mashariki itarekodiwa na Kampuni ya Wanene ambayo imekuwa ikifanya kazi nzuri na bora kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na kwingineko.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Wanene, Darsh Pandit amesema kuwa lengo la kampuni yake ni kukuza sanaa ya Kibongo na Afri kaMashariki kwa ujumlaambao wao wamedhamini kurekodi video ya mshindi atakayepatikana huku kigezo kikubwa kikiwa ni lazima mtayarishaji awe Mwafrika na video iwe na madhari ya nchi husika.

Video zilizoteuliwa kuingia katika kushiriki kinyang’anyiro hicho ni Umenikamata- Jux, Muziki ya Darasa ft Ben Pol na Natafuta Kiki ya Rayvan wa Tanzania, kwa Kenya ni Uko ya Avri, Now You Know ya Nyanshiski, Evarlast ya Gudi Gudi na Problem ya NaiBoi ambao kwa Uganda ni Jubilation ya Eddy Kenzo, SheebahKarungi ya Nkwatako, A Pass ya Gamululu ft Konshens.
Mwandishi Wetu