×

Nay: Godzilla Njoo Nikusaidie, Stress Zitakufanya Ule Unga!

 

Nay wa Mitego

STAA wa ngoma ya ‘Moto’ ambayo inafanya vizuri kwa sasa, Emmanuel Elibariki,  maarufu kwa jina  la Nay wa Mitego True Boy, ameamua kumkaribisha msanii Godzilla kwenye studio yake ya Free Nation iliyopo Sinza Kijiweni.

Godzilla

Nay ambaye amempiga kijembe Godzilla kwenye ngoma yake hiyo ya Moto kuwa kwa sasa ameshuka kimuziki na pengo lake limezibwa na msanii Billnass, kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika hivi:

“Ujinga ni kukasirika pale unapoambiwa ukweli, unapanic #MOTO watag waliopaniki na kubishana na ukweli, mimi naanza na kingzilla, ila Billnass una roho mbaya kijana hutaki kumpa hata upenyo kaka ako..! Njoo nikusaidie Kingzilla, maana stress ulizonazo utaja kula ngada bure, Karibu Free nation966, Tutakurudisha kwenye game”

Na Isri Mohamed

Leave a Comment