×

VIDEO: Shabiki Amvaa Wayne Rooney Uwanjani Mechi Ikiendelea

Shabiki akimvaa Rooney uwanjani.

 

MMOJA wa mashabiki wa Tanzania waliofika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam amejitoa ufahamu na kumvamia mshambuliaji wa Everton, Wayne Rooney kwa nia ya kumkumbatia wakati wa mchezo dhidi ya Gor Mahia ya Kenya ukiendelea uwanjani hapo.

Rooney naye akamkumbatia shabiki huyo.

 

Baada ya kitendo hicho ambacho amekifanya wakati mpira ukiwa umesimama kwa muda kufuatia mmoja wa wachezaji wa Gor Mahia kuumia na kulala chini, polisi walimvaa shabiki huyo na kumwondoa uwanjani humo mpesempese.

 

Hata hivyo shabiki huyo ameachiliwa huru kwa amri ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu Hassan aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mchezo huo.

TAZAMA VIDEO YA TUKIO HILO

TAZAMA MKWAJU WA ROPONEY UKIZAMA WAVUNI

 

Leave a Comment