×

Dickson Kagembe Aagwa na Mamia, Kuzikwa Bukene Tabora Kesho

Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kushoto mwenye tai nyeusi) na waombolezaji wengine wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu kuelekea kwenye gari tayari kwa safari kutoka Hospitali ya Muhimbili, Dar kuelekea mkoani Tabora kwa mazishi.

 

MAREHEMU Dickson Kagembe aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akisomea Sheria na baadaye akakumbwa na ugonjwa kansa ya damu (leukemia) ulioyachukua maisha yake jana kunako saa 2:45 jana katika Hospitali ya Muhimbili, leo ameagwa na mamia ya ndugu, jamaa na marafiki waliofurika katika Kanisa Katoliki, Muhimbili, lililoendesha misa ya kumuaga.

 

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers, Glory Casmir (kushoto) na Huruma Bujiku waiomboleza wakati wa kuaga mwili wa marehemu.

 

Siku Ambayo Shigongo Aliwakutanisha Wakonta na Dickson-Part 1

Dickson ambaye alikuwa ni ndugu mkubwa wa wafanyakazi wa kampuni ya Global Publishers, tangu Mkurugenzi Mtendaji wake, Eric Shigongo, kukutana naye wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Ocean Road, amesafirishwa leo kuelekea nyumbani kwao Bukene, Mkoa wa Tabora, ambapo atazikwa.

 

Abdallah Mrisho na wafanyakazi wengine wa Global Publishers wakiagana na kaka wa marehemu, Kagembe Boniphace (wa pili kushoto) kabla ya kuanza kwa safari kulekea Tabora.

 

Miongoni mwa watu waliofurika katika kumuaga ni jamii ya wanafunzi na wanachuo aliosoma nao na watu wengine waliomfahamu na kushirikiana naye katika mambo mbalimbali wakati wa uhai wake.

 

Katekista wa Kanisa Katoliki Parokia ya Muhimbili, Peter Ndomba akibariki mwili wa marehemu kwa maji ya baraka wakati wa ibada ya kuaga.

 

Watu wengine waliojumuika katika kumuaga Dickson ni watu mbalimbali ambao walikuwa wamejitolea kumsaidia kwa hali na mali wakati akipata matibabu hadi kufikia mwisho wa uhai wake, wakiwemo wafanyakazi wa Global Publishers.

 

Aliyekuwa Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Muro akipita kutoa heshima zake za mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa marehemu Dickson.

 

Wengi wa waombolezaji waliofika hapo, hususan wanafunzi wenzake, walishindwa kujizuia kumwaga machozi kuondokewa na mtu ambaye aliwahi kushika nyadhifa za uongozi wakati wakiwa naye katika shule za kawaida na chuo kikuu na akawaongoza kwa uadilifu na unyenyekevu.

 

Mmoja wa waombolezaji akiaga kwa huzuni.

VIDEO: Siku Ambayo Shigongo Aliwakutanisha Wakonta na Dickson-Part 2

Dickson aliyefariki akiwa na umri wa miaka 32 na ambaye amekuwa akipata matibabu ya ugonjwa huo kwa miaka ipatayo miwili, ameacha mke na watoto watatu. Bwana alitoa na Bwana ametwaa; jina lake lihimidiwe! Amina.

 

Mke wa marehemu, Julieth Mathias (katikati) akisaidiwa na waombolezaji wakati wa kuaga mwili wa mumewe.

 

Waombolezaji wakimpa pole kaka wa marehemu.

 

Waombolezaji wakilia kwa uchungu.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric James Shigongo (aliyesimama) akiwa na Dickson Kagembe (kulia) enzi za uhai wake na Wakonta Kapunda.

 

Eric Shigongo akimpa pole Dickson  enzi za uhai wake alipomtembelea katika Hospitali ya Ocean Road, Dar.
Mfanyakazi wa Global Publishers, Huruma Bujiku (kushoto) akiwa na Dickson Kagembe enzi za uhai wake.

 

RICHARD BUKOS NA WALUSANGA NDAKI | GLOBA PUBLISHERS.

Professional Gathering: Dickson Kagembe Alivyosimulia A-Z Kuhusu Aliyoyapitia Kwenye Maisha Yake

Leave a Comment