×

Mkazi wa Kigoma Aibuka Kidedea Droo Ndogo ya Tano ya Shinda Nyumba

Black Warriors wakitoa burudani viwanjani hapo wakati wa droo hiyo.

 

ILE droo ndogo ya tano ya shindano la Bahati Nasibu la Shinda Nyumba linaloendeshwa na Kampuni ya Global Publishers kupitia Magazeti ya Championi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi, Risasi Mchanganyiko, Amani na Uwazi imefanyika leo Alhamisi Julai 20, katika Viwanja vya Las Vegas vilivyopo Mabibo jijini Dar es Salaam.

 

Wasomaji wakikusana kuponi zao za shinda nyumba.

 

Katika droo hiyo, Geofrey Shangalawe (53) Mkazi wa Kigoma ameibuka mshindi wa Televisheni ‘flat screen’  mpya ambapo baada ya kupigiwa simu na MC Chaku aliyekuwa akiendesha droo hiyo, mshindi huyo hakuamini mara moja kama kweli ameshindia flat screen.

 

Kuponi zikichanganywa ili kumtafuta mshindi.

 

“Aaaaaa, aisee! TV nchi ngapi? Hahahaaa! Sina hata la kusema, mwanzoni nilidhani washindi wanapangwa tu, lakini kumbe siyo, siamini kama nimeshinda, nawashukuru sana Global. Niwaombe na wasomaji wengine wasikate tamaa maana hata mimi sikujua kama nitashinda siku moja,” alisema Shangalawe kwa njia ya simu.

 

Kuponi zikichanganywa ili kumtafuta mshindi.

 

Mdau akichukua kuponi moja katikati ya rundo la kuponi ili kumpata mshindi.

 

Washindi wengine waliopatikana katika droo hiyo ni pamoja na Festo Masagasi mkazi wa Bunju jijini Dar aliyejishindia Smart Phone mpya aina ya Tecno, Salome Msaru wa Mtwara na Ummysalama Sasha wa Dar ambao wote waliibuka washindi wa vyombo vya nyumbani (dinner set).

 

MC Chaku akishirikiana na mdau kusoma jina la mshindi.

Mwingine ni Anthony Thomas mkazi wa Mabibo jijini dar aliyejishindia fulana mpya ya shinda nyumba.

Kuponi zikichanganywa.

Kutokana uwazi uliofanyika katika zoezi zima la uchezeshwaji wa bahati nasibu hiyo hata alipotajwa mshindi wa mwisho umati huo ulionekana kushangilia na kuyakubali matokeo hayo huku wengine wakiahidi kuzidi kushiriki mchezo huo ambapo siku ya mwisho mshindi ataibuka na nyumba mpya yenye fenicha zote ndani.

MC Chaku akimpigia simu mshindi.

Shindano hilo linadhaminiwa na King’amuzi cha Ting, British Schools pamoja na Kampuni ya Simu za mkononi ya Tecno.

Mdau aliyefungwa uso akiruhusiwa kuchanganya kuponi na kuchagua moja ya mshindi.

 

Kutoka kushoto ni Mhariri wa Uwazi, Elvan Stambuli, Msimazi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Bakari Majjid na Mhariri wa Ijumaa Wikienda, Sifael Paul.

 

PICHA NA RICHARD BUKOS | GLOBAL TV ONLINE

 

Leave a Comment