
TAMASHA la Castle Lite Unlocks lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar usiku wa kuamkia leo wasanii wa ndani ya Tanzania na nje waliandika historia kwa kupiga shoo kali wakiongozwa na msanii Future kutoka Marekani na Refiloe Maele Phoolo ‘Cassper Nyovest’ kutoka Afrika Kusini.
Mashabiki walijitokeza kwa wingi katika viwanja hivyo huku wakimshangilia kila msanii aliyekuwa akipanda stejini kutoka shoo hiyo ya aina yake iliyoandaliwa kwa mbwembwe nyingi.
Wasanii waliofanya shoo katika tamasha hilo ni: Weusi, Vee Money, Navy Kenzo, Rosa Ree, Cassper Nyovest kutoka Afrika Kusini na msanii kutoka Marekani, Future, na wengineo.




1 Comment