
Manchester United imeshinda kwa penalti 2-1 dhidi ya Real Madrid katika mechi za michuano ya ICC iliyopigwa jijini California, Marekani.

Ndani ya dakika 90 timu hizo zilimaliza kwa sare ya 1-1 baada ya Jesse Lingard kutangulia kufunga na baadaye Casemilo akaisawazishia Madrid.

Mechi hiyo iliyokuwa na mvuto wa aina yake De Gea alishuhudiwa akiokoa mikwaju ya penati na kuipa ushindi klabu yake ya Man U.

Anthony Martial alitumia juhudi binafsi na kumtengenezea pande Jesse Lingard na kuandika goli la kwanza.

Casemiro aliisawazishia Madrid kwa njia ya penalti baada ya mlinzi mpya wa United Victor Lindelof kumuangusha Theo Hernandez katika eneo la hatari. Penalti saba kati ya kumi hazikuingia nyavuni.

REAL MADRID (4-3-3): Navas; Carvajal (Hakimi 46), Varane (Quezada 46), Nacho (Manu 46), Marcelo; Modric (Kovacic 46), Kroos, Isco (Oscar 46); Vazquez (Hernandez 46), Benzema (Gomez 46), Bale (Franchu 46). Subs: Tejero, Gomez, Casilla, Mayoral, Zidane, Yanez.

MAN UTD (4-1-4-1): Romero (De Gea 46); Fosu-Mensah (Blind 46), Bailly (Smalling 46), Jones (Lindelof 46), Darmian (Valencia 77); Carrick; (Pogba 46) Lingard (Mkhitaryan 46), Fellaini, A Pereira (Herrera 46, McTominay 52), Martial; Rashford (Lukaku 46). Subs: Tuanzebe, J Pereira, Valencia, Mitchell.

Mabao ndani ya dakika 90: Lingard (dakika ya 45) na Casemiro (dakika ya 69) kwa penalty.
