×

Hapi Amaliza Mgogoro wa Ardhi Nyakasangwe

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi, akizungumza na wakazi wa Nyakasangwe.
…Akisisitiza jambo katika mazungumzo hayo.
Baadhi ya wananchi wa Nyakasangwe wakimsikiliza.

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi, ametoa miezi mitatu kwa kampuni ya upimaji wa ardhi ya Afro Map kuhakikisha wanamaliza upimaji wa ardhi kwa eneo la Nakalekwe, Mtaa wa Nyakasangwe, Kata ya Wazo, ambalo limekuwa na mgogoro kwa muda wa zaidi ya miaka kumi.

 

Hapi amesema chanzo cha mgogoro wa eneo hilo ni kutokupimwa, hivyo atahakikisha maeneo yote katika wilaya yake yanapimwa ili migogoro ya ardhi iwe historia kwa wakazi wa Kinondoni.

 

Aidha Hapi ameeleza kuwa serikali haiwezi kuacha wakazi zaidi ya 3,000 kupoteza maeneo yao  kwa kutokuwepo hati maalum za wamiliki  na hivyo maeneo hayo yatapimwa kisheria na kupatiwa hati halali.

 

Aidha ametoa onyo kwa matapeli wanaouza ardhi pasipokuwa na vielelezo sahihi na kuagiza taarifa zao ziwe zinafikishwa mapema sehemu husika ili hatua kali ziwe zinachukuliwa dhidi yao.

 

Kwa upande wake, diwani wa Kata  ya Nyakasangwe, Joel Mwakalebela,  ameipongeza kamati ya wananchi wenye mashamba iliyoundwa kwa juhudi kubwa ya kukaa pamoja na kutaua migogoro iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa eneo hilo.

 

NA DENIS MTIMA/GPL

 

Leave a Comment