×

Rasmi Mbio za Rotary Dar Marathon zazinduliwa

Mwenyekiti wa Rotary Dar Marathon, Shamila Batt (kushoto) na Mkurugenzi wa Benki M, Jacqueline Woiso wakisaini mkataba wa makubaliano wakati wa uzinduzi wa Rotary Dar Marathon
Mwenyekiti wa Rotary Dar Marathon, Shamila Batt (kushoto) akikabadilishana mkataba na Mkurugenzi wa Benki M, Jacqueline Woiso mara baada ya kuisani wakati wa uzinduzi wa Rotary Dar Marathon
Wakiwa katika pamoja na wajumbe mara baada ya uzinduzi
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Rotary Dar Marathon, Catherinerose Barreto akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani
Mkurugenzi wa Benki M, Jacqueline Woiso akizunguma jambo mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi huo
Shamila Batt akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi huo

KLABU saba za Rotary za jijini Dar kwa kushirikiana na Benki M mapema leo Jumatano zimefanikiwa kuzindua mbio na matembezi ya Rotary Dar Marathon zitakazofanyika Oktoba 14 mwaka huu kwenye Viwanja vya Greens Oysterbay jijini Dar.

Mbio hizo mwaka huu zitafanyika kwa mara ya tisa mfululizo tangu kuanzishwa kwake zikiwa na lengo kuu la kuchangisha fedha kwa ajili ya shughuli za kijamii.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo, Catherinerose Barretto alisema kuwa wana furaha kubwa ya kuzindua na kusaini mkataba na mdhamini mkuu wa Benki ya M katika mbio na Matembezi ya mwaka huu ambayo yatakuwa ni ya aina yake.

“Tunayo furaha ya kuzindua na kusaini mkataba kwa kushirikiana na mdhamini wetu mkuu Benki M katika mbio na matembezi ya mwaka huu. Kuna mambo mapya yameongezeka kwa washiriki, tutakuwa na mbio za KM 42 ambazo ni full Marathon, baiskeli kutoka KM 21 za mwaka jana hadi KM 42, matembezi kutoka KM 9 hadi KM 10 na KM 5 matembezi ya kawaida.

“Mwaka huu tutakuwa na Marathon nzima tofauti na miaka iliopita lakini pia tumelenga kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya katika hospitali ya CCBRT ambayo huhudumia wananchi wenye matatizo mbalimbali ya ulemavu ili kuwezesha hospitali hiyo kutoa huduma kwa wananchi wengi na fomu kwa washiriki zitakuzwa kwa bei ya shilingi 35000 kwa wakubwa na watoto itakuwa ni 10000,” alisema Barreto.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Benki M, Jacquleline Woiso alisema kuwa: “Tumekuwa washiriki katika shughuli za mbalimbali za maendeleo ya kijamii na tumekuwa tukishirikiana na Rotary katika Rotary Dar Marathon tangu ilipoanzishwa mwaka 2009, naamini kwa pamoja tutashirikiana kufanikisha ujenzi wa kituo cha afya cha hapo CCBRT.”

Na Ibrahim Mussa|GPL

Leave a Comment