×

‘DOGO’ APATA BONGE LA ZALI BAADA YA KUBETI, ALAMBA MIL 284

 

'DOGO' APATA BONGE LA ZALI BAADA YA KUBETI, ALAMBA MIL 284
…Kikuba Ramadhan akiwa na mfano wa hundi wa fedha alizojishindia.

MSHINDI wa michezo ya kubahatisha kutoka mkoani Singida, Kikuba Ramadhan Kimu amejishindia kitita cha  shilingi milioni 284 baada ya kubeti kupitia M-Bet inayoendesha msimu wake wa pili uitwao Perfect 12.
Akizungumza kwa furaha wakati wa makabidhiano ya fedha zake yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, mshindi huyo amesema amefurahishwa sana na ushindi huo kwani hakutarajia kama anaweza kuibuka mshindi na kuongeza kuwa fedha hizo zitamwezesha kufanya biashara mbalimbali.

'DOGO' APATA BONGE LA ZALI BAADA YA KUBETI, ALAMBA MIL 284
Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe akifafanua jambo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Naye msemaji wa kampuni inayoendesha mchezo huo, Godhele Wambura alisema: “Kupitia ushindi huu nawaomba Watanzania wote wafahamu kuwa mchezo wa kubet ni wa uwazi na haki, wala hakuna mtu anayeweza kufanya wizi kupitia mchezo huu.

“Watambue kuwa tunauendesha kwa kufuata taratibu zote za nchi na ndiyo maana leo tumeweza kumkabidhi hundi ya shilingi mil. 284 mshindi huyu na tutazidi kutoa zawadi kwa washindi kupitia msimu huu.”

'DOGO' APATA BONGE LA ZALI BAADA YA KUBETI, ALAMBA MIL 284
Msemaji wa mchezo huo wa bahati nasibu ya M.Bet, Godhele Wambura (kushoto) akimkabidhi hundi Kikuba Ramadhan aliyejishindia kitita hicho.

Akizungumza katika hafla hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe  amewaasa Watanzania kuendelea kushiriki katika michezo hiyo ya kubahatisha kwani bodi yao inasimamia kwa ufasaha hivyo haki zote zipo wazi wala hakuna mahali ambapo hawafuatilii hivyo hawezi kukubali mtu akapitisha mwanya wowote wa wizi ili waweze kunufaika.

'DOGO' APATA BONGE LA ZALI BAADA YA KUBETI, ALAMBA MIL 284
Kikuba akiwa na ndugu zake kwenye hafla hiyo.

Leave a Comment