×

FT: YANGA 3-2 SINGIDA UNITED, UWANJA WA TAIFA

Wachezaji wa Singida United wakipasha katika mazoezi.

FULL TIME

Mwamuzi anamaliza mchezo, Yanga wanaibuka na ushini wa mabao 3-2, awali Yanga walikuwa nyuma kwa mabao 2-1 lakini wametoka nyuma na kupata ushindi.

Dakika ya 91: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!

Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 3 za nyongeza.

Dakika ya 86: Matokeo sasa ni 2-2, furaha imerejea kwa mashabiki wa Yanga hapa uwanjani.

Tambwe anafunga, kipa anapambana kuufuata mpira lakini anashindwa kuudaka, unajaa wavuni.

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Amissi Tambwe anaendaka kupiga penalti.

Dakika ya 83: Kipa wa Singida anashika miguu mshambuliaji wa Yanga aliyekuwa akielekea kufunga.

Yanga wanapata penaltiiiii

Dakika ya 80: Kenny Ally wa Singida anapewa kadi ya njano kwa kuchelewesha kucheza mpira uliokuwa umetoka.

Dakika ya 65: Ajibu anachukua mpira kutoka pembeni lakini anatoa pasi mapema.

Dakika ya 64: Kasi ya mchezo imepungua kiasi.

Dakika ya 60: Ibrahim Ajibu anawekwa chini na Deus Kaseke wakati walipokuwa wakiwania mpira.

Dakika ya 55: Washambuliaji wa Singida wanaonekana kuwa na mbinu nyingi, wanawapa upinzani Yanga.

Dakika ya 54: Kila mara Singida wanapofanya jambo zuri mashabiki wanaodhaniwa kuwa ni wa Simba wanashangilia.

Dakika ya 50: Yanga wanatulia na kumiliki mpira kwa dakika kadhaa sasa.

Kipindi cha pili kimeanza kwa kasi, Yanga wanaonakana wanatafuta bao la kusawazisha kwa nguvu

Kipindi cha pili Kimeanza

MAPUMZIKO

Dakika 45 +2 Mwamuzi anapuliza filimbi kukamilisha kipindi cha kwanza, Yanga wapo nyuma kwa mabao 2-1

Dakika 43: Kipa wa Yanga, Beno Kakolanya anafanya kazi ya ziada.

Dakika ya 42: Yanga wanaonekana kutafuta bao la kusawazisha kwa nguvu zote.

Dakika ya 35: Yanga wanakosa bao la wazi kipa wa Singida United anaokoa kwa kupanchi.

Dakika 29;  Timu zote zinashambuliana kwa zamu bado Yanga 1- 2 Singida United

Dakika 27: Singida United wanapiga faulo kuelekea lango la Yanga, Ynaga wanaokoa.

Goooooooooooooo Singida United wanapata bao la pili

Dakika ya 19: Bado matokeo ni 1-1 timu zote zinashambuliana kwa zamu  Kelvin Yondani anafanya kazi kuwadhibiti washambiliaji wa Singida United.

Dakika ya 14; Singida United wanakosa bao la wazi kabisa, Yondani anatoa nje.

Dakika 13; Yanga wanamiliki mpira na kufanya mashambulizi mara kwa mara

Dakika ya 6: Yanga 1-1 Singida united mchezo upo sepeed sana wanashambuliana kwa kazi

Sigida  United wamekosa penalti baada ya mchezaji wao kuangushwa ndani ya bosi. Singida United wamepiga penalti wamekosa.

KIKOSI:

1. Youthe Rostand

2. Juma Abdul

3. Haji Mwinyi

4. Kelvin Yondani

5. Abdallah Shaibu ‘Ninja’

6. Thaban Kamusoko

7. Burhani Yahya

8. Raphael Daud

9. Amiss Tambwe

10. Donald Ngoma

11. Ibrahim Ajibu

 

SUB:

Beno Kakolanya

Hassan Kessy

Nadir Haroub

Andre Vicent

Juma Mahadhi

Yusuf Mhilu

Edward Martin

Leave a Comment