




Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Anayeshughulikia Muungano na Mazingira, January Yusuph Makamba, leo Jumatano alitembelea ofisi za Global Publishers na kupata nafasi ya kuwasalimia wafanyakazi. Katika mazungumzo yake mafupi ofisini hapo, waziri alisisitiza uwepo wa mikakati mizuri ya kuendelea kuboresha mazingira na kuudumisha muungano.
Aidha Waziri Makamba amewasisitiza Watanzania kuendelea kuiunga mkono serikali ya Rais John Pombe Magufuli katika kuboresha mazigira ili kuifanya Tanzania iendelee kuwa nchi yenye amani na mazingira bora.