×

Polisi Wakabiliana na Wafuasi wa Odinga Kisumu

Polisi wakitoa mawe barabarani baada ya kupambana na wafuasi wa uapinzani.

Polisi wa kukabiliana na ghasia nchini Kenya wamekabiliana na vijana waliokuwa wanaandamana na kufunga barabara katika mtaa wa Kondele mjini Kisumu.

Mfuasi wa Raila akiwa na bango.

Maeneo mengine ya mji huo ambao ni ngome ya mgombea wa upinzani, Raila Odinga, hayakuwa na watu wengi huku biashara nyingi zikifungwa.  Mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza amesema polisi walifyatua risasi  hewani kujaribu kuwatawanya waandamanaji.  Polisi wameingia pia katika baadhi ya mitaa ya mji huo kufanya doria.

 

Tazama hali ilivyokuwa kupitia picha za Peter Njoroge:

Waandamanaji wakiendelea kupambana na polisi.
Polisi wakiwa wametanda mitaani.

Leave a Comment