×

Airtel, Veta Wazindua Namba Maalum Kuwahudumia Wanafunzi

Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam Habibu Bukko akipeana mikono na Meneja Uhusiano Airtel Tanzania baada ya kuzindua namba maalamu ya kuwahudumia wanafunzi wa VSOMO.
 
Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi Tanzania (VETA) kwa kushirikiana Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mradi wa Airtel FURSA wameendeleza mkakati wao wa kuendelea kusambaza elimu ya ufundi stadi nchini kupitia mpango wao wa VSOMO App kwa kuzindua namba maalum zitakazowafanya wateja au wanafunzi wanaojiunga na huduma ya Masomo kupitia Application ya VSOMO kupata maelekezo kupitia namba hiyo pindi wanapokwama na kuhitaji maelekezo ya haraka.
 
Akiongea katika hafla ya kutangaza namba hiyo Mkuu wa Kanda wa  chuo cha VETA nchini Habibu Bukko alisema;
“ Tunafuraha sana sasa tunapata suluhisho lakuwa na namba maalum ambapo mwanafunzi anaweza kupiga simu na kupata maelezo muhimu ya masomo, VETA lengo letu ni kuendelea kuwawezesha watanzania kushiriki vyema kiutendaji katika sera ya uchumi wa Viwanda, VETA kupitia huduma tunayotoa kupitia VSOMO tumeshirikiana tena na Airtel kwa kuhakikisha kuwa masomo ya Vsomo yanawafikia wengi “
Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya kuzindua namba maalum ya kuwahudumia wananafunzi wa VSOMO. Kulia Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam Habibu Bukko na Mkuu wa VETA Kipawa Mhandisi Lucias Luteganya (kati kati).

 

 “Tunazindua namba hii 0699859573 na 0699859572 zitakazowawezesha wanafunzi wenye nia ya kutaka kusoma kupitia mfumo wa VSOMO kuweza kukamilisha malengo yao bila kikwazo chochote kwa kuuliza na kusaidiwa muda wowote tunapokuwa wazi” alisisitiza Bw. Bukko.
Nae  Mkuu wa Chuo cha Veta Kipawa ambae ndie msimamizi wa mpango wa VSOMO  Eng. Lucias Luteganya alisema “Namba hizo maalum zitahudumia wanafunzi au yeyote atakaepiga ili kupata msaada wa VETA kwa siku zote saba za wiki kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni”.
“Tumeona kuna umuhimu wa kuweka namba hii iweze kuwahudumia hasa kwa kipindi hiki ambacho mpango huu wa Vsomo unazidi kupanuka kwa kuongeza kozi nyingi kulingana na mahitaji” alieleza Eng, Luteganya
Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam Habibu Bukko akiongea na waandishi wa habari baada ya kuzindua namba maalum ya kuhudumia wanafunzi wa VSOMO. Kushoto ni Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya alisema “Airtel tunaendelea kujisikia fahari kwa  kufanikiwa kuogeza ubunifu katika huduma zetu kila wakati,  tunajionea  VSOMO ikiendelea kutoa suluhisho na kuongeza tija kwa jamii kwa kuwawezesha wanafunzi wengi kupata elimu hasa waliopo maeneo ambayo VETA haina kituo, hivyo basi uzinduzi wa namba hizi maalum ni suluhisho lingine lakuendelea kurahisisha upatikanaji wa elimu ya Ufundi stadi ili tupate wataalamu wakutosha katika sekta mbalimbali.
“Namba hizi zitapatikana siku zote za kazi kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa10 jioni ambapo kila simu itakayopigwa itakuwa na gharama ya shilingi 60 tu na mteja hatapangiwa muda wa kuongea na mtoa huduma hadi mwisho wa kuhudumiwa.
 
Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam Habibu Bukko akipeana mikono na Meneja Uhusiano Airtel Tanzania baada ya kuzindua namba maalamu ya kuwahudumia wanafunzi wa VSOMO.

 

“Vile vile ili kupata maelezo ya kutosha mwanafunzi anaweza kutembelea kurasa zetu za mtandao ya kijamii pamoja na website ili kupata maelekezo ya VSOMO wakati wowote ”
VSOMO hutoa wa mafunzo ya Ufundi stadi kwa njia ya simu za mkononi hivyo kufanya simu ya mkononi kuwa Darasa, hivi karibuni VETA wameongeza kozi  mpya katika mfumo wa vsomo ikiwemo ya  Huduma ya chakula na mbinu za kuhudumia wateja, Matengenezo ya kompyuta,umeme wa viwandani, ufundi Bomba wa Majumbani, Umeme wa magari, kutengeneza na kupamba keki, ufundi wa simu, ufundi pikipiki, Utaalamu saluni na urembo, ufuni wa kuchomelea pamoja na ufundi wa Aluminium
Mfumo huu wa masomo kwa njia ya Mtandao VSOMO, sasani maarufu kwa vijana ambapo takwimu zinaonyesha zaidi ya vijana 30,000 tayari wamepakua application ya VSOMO kupitia simu zao za Androad BURE, na wengine 8000 wamejiandikisha kusoma.

Leave a Comment