×

BOB JUNIOR AELEZA KILICHOMPOTEZA KWENYE MZIKI

Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’.

MSANII wa Bongo Fleva ambaye pia ni prodyuza, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’ ameibuka na kueleza kilichompoteza kwenye muziki huku akijikuta akipitwa na wale wanamuziki aliowafundisha au kuwaingiza kwenye tasnia hiyo akiwemo Bonge la Nyau.

Akipiga stori na Mikito Nusunusu, Bob Junior alisema ni kweli amepitwa na amepotea kwenye ulimwengu wa muziki kwa sababu aliamua kuingia kwenye biashara ambapo mpaka sasa anamiliki maduka mawili Kariakoo huku akiwa anasimamia mali za wazazi wake kwa kuwa ndiye mtoto wa kwanza.

“Ninafanya biashara ya kupeleka bidhaa mbalimbali nchi tofautitofauti na pia namiliki maduka mawili Kariakoo hivyo nakuwa bize sana ndiyo maana nimepotea kwenye muziki ila wiki ijayo nitaanza kuachia ngoma mpya,” alisema Bob Junior.

STORI: GLADNESS MALLYA| RISASI JUMAMOSI

 

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

——-

Shamrashamra Mapokezi ya Watoto wa Shule ya Lucky Vincent KIA

Leave a Comment