Mkali wa Bongo Fleva, Ericom ameiachia video yake mpya ya wimbo wa Danijah ambao ameufanyia katika Studio za AM Record za jijini Dar, chini ya Mtayarishaji Bob Maneck ambaye ngoma zake nyingi zinafanya vizuri kwenye game.
Akizungumza na GPL, Ericom amesema kuwa amejipanga kuwapa vitu vikali mashabiki wake kwa sababu ana uwezo mzuri wa kufanya kazi nzuri kulingana na mahitaji ya soko.
“Mashabiki wangu wanipe ushirikiano ili niendelea kuwapa vitu vizuri kwani mawe mazuri yapo yakutosha,”alisema Ericom.