×

Ajali ya Treni na Coaster Morogoro, Mganga Mkuu Anena

Eneo la tukio.

IKIWA imepita takribani miezi mitatu tangu wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent ya Mkoani Arusha wapate ajali na watu 35 kupoteza maisha, leo majira ya saa moja asubuhi, treni ya abiria iliyokuwa ikitokea Bara imegongwa na basi la abiria aina ya Coaster lenye namba za usajili T 438 ABR katika eneo la TANESCO, mjini Morogoro.

Daladala iliyopata ajali.

Coaster hiyo inayofanya safari zake kati ya Morogoro mjini na Kihonda ilikuwa imebeba wanafunzi wa shule tofauti wakielekea shuleni, mmoja wao anadaiwa kupoteza maisha huku wengi wao wakijeruhiwa kutokana na ajali hiyo tofauti na taarifa zilizosambaa mwanzo kuwa watu watatu walikuwa wamefariki.

Wananchi wakilisukuma gari hilo.

Baada ya kuwatoa majeruhi na maiti, polisi kwa kushirikiana na wananchi walilisukuma daladala hilo hadi bondeni na kuipisha treni kuendelea na safari yake.

Hali ilivyokuwa eneo la tukio.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini humo, Mganga Mkuu wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dkt. Frank Jacob amesema leo asubuhi amepokea maiti ya mwanafunzi mmoja na majeruhi kadhaa ambapo wawili kati yao hali zao ni mbaya.

Treni ikipita.

Baada ya kutokea kwa ajali hiyo mwandishi wetu alifika haraka eneo la tukio na kukuta umati mkubwa wakimshushia kichapo dereva wa daladala hiyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja wakati akitaka kukimbia baada ya tukio hilo.

VIDEO YA TUKIO HILO

Gari likiwa limebinuka baada ya kusukumwa na wananchi kupisha treni.

Umati wa wananchi wa Morogoro umejazana nje ya hospital hiyo kwa lengo la kuwashuhudia majeruhi hao, pia uongozi wa Mkoa wa Morogoro upo hospitalini hapo.

Ndugu na jamaa waliofika Hospitali ya Rufaa Morogoro.

Na Dustan Shekidele | GPL| Morogoro

 

Breaking News: Chadema Wafunguka Lissu Aachiwe, Ngeleja Akamatwe