×

Makamu wa Rais Dkt. Mpango Amuwakilisha Rais Samia Mwanza

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akiagana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Mhashamu Maimbo William Mndolwa wakati alipomuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye Sherehe ya kuwekwa Wakfu Askofu wa Tano wa Dayosisi ya Victoria Nyanza, iliyofanyika leo Mei 16,2021 katika Kanisa la Anglikana Jijini Mwanza.kulia ni Mama Mbonimpaye Mpango.
Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, akihutubia Waumini wa Dini ya Kikristo na Watanzania.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, akisalimiana na Baadhi ya Maaskofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania.

(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwenye Sherehe ya kuwekwa Wakfu Askofu wa Tano wa Dayosisi ya Victoria Nyanza, iliyofanyika leo Mei 16,2021 katika Kanisa la Anglikana Jijini Mwanza.

Leave a Comment