×

SITASAHAU NILIPOLALA NA MWANAMKE JUU YA KABURI (14)

SITASAHAU NILIPOLALA NA MWANAMKE JUU YA KABURI (14)

 

ILIPOISHIA…

Nilifanikiwa kupata usingizi kiasi. Ulikuwa usingizi wa mang’amung’amu. Usingizi wangu ulijawa na ile shauku ya kuujua ukweli giza litakapopotezwa na nuru. Nilitabasamu kidogo kwa sababu mzee niliyekuwa nikimtafuta, kesho ningekutana naye katika gereza nililomwona ili ayamalize matatizo yangu.

 

ENDELEA KUISOMA…

 

Asubuhi ilifika. Jogoo liliwika kama halitaki. Nilitamani kuamka ili niende mapema gerezani kuuliza habari za Mzee Samike. Lakini nilipotaka kuinuka, akili ikaniambia pata usingizi wa kutosha. Lala kidogo utaamka baadaye. Nikalala.

 

Nilishtuka saa nane mchana. Haukuwa usingizi wa kawaida. niliiogopa hali hiyo lakini sikujali. Nikajiandaa harakaharaka kisha nikaianza safari ya kwenda gerezani.

 

Nilifika gerezani. Kama nilivyowaza awali, haikuwa siku ya kuwatembelea wafungwa. Sikujali. Nikamsogelea askari mmoja aliyesimama imara pembezoni mwa ukuta mnene wa jela.

 

“Habari yako afande,” nilitoa salamu. Afande akageuka. Alikuwa mweusi ti, kama kipande cha giza, meno meupe yaliyoacha mwanya mpana mfano wa pengo na kichwani alifanana na sufuria kwa ule ukubwa wa kichwa chake. Kilichonimaliza nguvu ni kwamba, alikuwa ni yule askari wa jana ambaye alinitega nikadondoka kisha akanifukuza… BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Leave a Comment