×

SITASAHAU NILIPOLALA NA MWANAMKE JUU YA KABURI (15)

SITASAHAU NILIPOLALA NA MWANAMKE JUU YA KABURI (15)

 

ILIPOISHIA…

Nililala usingizi wa matumaini. Niliamini ni lazima ningempata Samike. Nikiwa usingizini, niliota mseto wa ndoto za zamani na mpya. Katika ndoto mpya iliongezeka sura ya askari. Nilikiota kichwa chake. Nikawa kama naogelea katika ndoto za masufuria. Nilipoota kuhusu kufukuzwa, nilipiga makelele. Kama kawaida yao, wazinzi wakashtuka wakidhani ni fumanizi. Walipogundua ni mimi, kama ilivyo siku zote wakanipuuza. Mchezo wa nyama ukaendelea.

 

ENDELEA KUISOMA…

Niliamka nisiye na matumaini. Nikawaza namna ya kumpata Mzee. sikupata jibu! Lilinijia wazo la kuanza upya msako. Nikalikubali wazo hilo. Baada ya kujiandaa, nikaingia barabarani kumsaka mzee.

 

Kila mtu niliyekutana naye nilimuuliza, “Umemuona Mzee katoka jela leo?” majibu yalikatisha tamaa na kuvunja moyo. Hakuna aliyemwona Samike.

 

Nilirejea saa nne usiku nikiwa nimechoka. Mbwa mchafu akabweka aliponiona. Hapo nikapata sehemu ya kupoza hasira, nilimporomoshea matusi mazito yaliyomkata mdomo, akabaki kimya!

 

Chumbani nililala bila kusafisha kitanda. Nikiwa nusu kusinzia nusu kuamka, niliamua kusitisha msako wa Samike. Nikaamua kurejea nyumbani ifikapo asubuhi. Mtu yule wa ajabu aliyenikimbiza nikaapa kutokumkimbia tena. “Nitasimama anichinje na upanga wake wenye makali kuwili,” niliwaza kishujaa… SOMA ZAIDI

Leave a Comment