
KUNA historia nyingi zipo na zinawekwa nchini Tanzania tangu pale taifa lilipopata uhuru, Desemba 9, 1961. Mojawapo ya historia zinazoelekea kuwekwa ni ile itakayotokea Septemba 27, mwaka huu na mpendwa msomaji, haujachelewa kuwa mtu wa kuiweka.
Siku hiyo, ambayo itakuwa ni Jumatano, itakuwa ni ya kipekee, kwa sababu mtu mmoja, ambaye hadi sasa hajijui, ambaye kuna uwezekano mkubwa ukawa ni wewe, ataamka akiwa kama alivyo, lakini majira ya jioni, atajikuta akikabidhiwa nyumba kubwa, yenye thamani ya mamilioni, ikiwa na hati kabisa!
Ni katika droo kubwa ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili, ambayo inaendeshwa na Global Publishers itakayochezeshwa ili kumpata mshindi wa kwanza baada ya washindi zaidi ya 30 wa zawadi ndogondogo kupatikana katika droo ndogo tano zilizochezeshwa maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam. Ni takribani siku 12 tu zimebaki ili kuifi kia Jumatano hiyo ya kihistoria na ingawa muda unaonekana kuwa mfupi, lakini bado ni mwingi kiasi cha kuweza kumshangaza kila mmoja. Kampuni bado inapokea kuponi kutoka kwa wasomaji wa magazeti ya Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi, Amani, Uwazi na Championi, ambayo ndiyo yanayochapishwa na Global Publishers.
Cha kufanya, baada ya kununua moja ya magazeti haya, kata kuponi zilizopo katika kurasa za pili na kujaza kwa jinsi ilivyoelekeza, halafu zipeleke kwa mawakala wetu walio kila kona nchi nzima ambao wataziwasilisha makao makuu ya kampuni, au kwa wale wakazi wa Dar, wazipeleke moja kwa moja katika Ofi si za Global Publishers, zilizopo Bamaga, Mwenge. Hakuna kuponi hata moja ambayo haitaingia katika pipa kubwa siku ya droo, zikiwemo zile zitakazokatwa katika magazeti ya Septemba 26, hivyo nafasi yako ya kushiriki bado ni kubwa katika kuibuka mshindi. Nyumba hii iliyojengwa Bunju A, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, itakuwa ni ya pili kutolewa na Global Publishers baada ya kufanya hivyo mwaka jana, ambapo mjasiriamali Nelly Mwangosi, mwenyeji wa Iringa aliibuka mshindi na kujipatia nyumba ambayo imejengwa eneo la Salasala jijini Dar. “Tumekamilisha kila kitu, kilichobakia sasa ni kuwaomba wasomaji wa magazeti yetu ya Ijumaa Wikienda, Amani, Uwazi, Risasi, Championi na Ijumaa kukata kuponi zao za mwishomwisho na kuzituma kwetu haraka iwezekanavyo. Kwa wale wa mikoani, kuponi zao wazipeleke kwa wakala wetu ambao wako kila sehemu nchini.
“Kwa wale wa Dar wazilete kuponi zao katika ofi si zetu zilizopo Bamaga, Mwenge na wazikabidhi kwa watu maalum wanaozipokea. Huu ni wakati wa kuhakikisha hawakosi nakala zao kwa vile muda umeshaisha. Wiki
mbili zilizobaki wahakikishe hakuna mtu anayeziacha kuponi zake bila kuzileta kwetu, kwa sababu huenda ile utakayoiacha nyumbani, ndiyo iliyokuwa ya mshindi,” alisema Abdallah Mrisho, ambaye ni Meneja Mkuu wa Global Publishers, alipotakiwa kueleza hatua ambayo wamefi kia hadi sasa.
Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili inafanyika baada ya kuwepo kwa droo ndogo tano zilizochezeshwa katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam ambako zaidi ya wasomaji 30 wa magazeti ya Championi, Ijumaa, Risasi, Uwazi, Amani na Ijumaa Wikienda waliibuka na zawadi za aina mbalimbali zikiwemo pikipiki, televisheni kubwa, simu za kisasa za mikononi, dinner set na ving’amuzi.