×

RC, Gambo apunguza kero za wananchi Arumeru

MKUU wa Mkoa wa Arusha
Gambo akizungumza na wananchi.
MKUU wa Mkoa wa Arusha
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo.

MKUU wa Mkoa wa Arusha

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ametoa msaada wa mifuko 200 ya saruji na nondo tani mbili, kwa ajili ya ujenzi wa daraja linalounganisha vijiji vya Kambi ya Maziwa na Sovowo, Arumeru Magharibi mkoani humo.

Gambo ametoa msaada huo katika mkutano wa hadhara na wanachi wa vijiji hivyo, uliofanyika katika Kijiji cha Ngorbob, Arumeru ambapo mbali na mambo mengine, amewashukuru wananchi hao kwa namna wanavyotoa ushirikiano katika shughuli za kijamii na kuzuia uhalifu.

Mkuu huyo wa mkoa yupo kwenye ziara ya kikazi ya siku tano katika Wilaya ya Arumeru kusikiliza kero na matatizo ya wananchi wa mkoa wake.

NA HILARY DAUDI/ ARUSHA

Leave a Comment