×

QUICK ROCKA : VIJANA WANGU NI WAKALI KWA HIPHOP TANZANIA NZIMA

Msanii wa miondoko ya Hip Hop Quick Rocka.

MSANII wa miondoko ya Hip Hop Quick Rocka anayetamba na wimbo wake mpya wa STILL,  ambaye pia ni meneja wa kundi la OMG na mmiliki wa studio ya Switch Studios Company, amefunguka juu ya watu  wote wanaochana hapa nchini na kusema  hamna msanii anayeweza kuchana zaidi ya wasanii wake wa OMG.

 

Na alipoulizwa juu ya watu wanaochana hapa nchini alifunguka haya: “Kwenye kizazi hiki sasa hivi hamna rapa kama vijana wangu wa OMG, ndo wanafanya Hiphop,  ukiacha hao hamna mwingine anayeweza kuwapiku.”

 

Kila meneja anayesimamia wasanii wake lazima atawasifia, hata ukiangalia meneja wa makundi ya Mkubwa na Wanawe, Yamoto Band na TMK ambaye ni  Said Fela,  hawezi kusifia kundi  jingine zaidi ya vijana wake.

NA : SAMSON JEREMIAH/GPL

Leave a Comment