RAIS wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. John Pombe Magufuli leo anawatunuku kamisheni maofisa wa Jeshi la Wanchi nchini. Tukio hilo linafanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
Maofisa hao 422 wataanza na cheo cha Luteni USU ambapo watakuwa na nyota moja. Ni Rais pekee ndiye mwenye mamlaka ya kutunuku kamisheni hiyo na si mtu mwingine.
Rais Magufuli amewatunuku Kamisheni ya LUTENI USU maofisa 422 wa JWTZ waliomaliza mafunzo yao, ambapo kati yao 32 ni wa kike na 390 ni wa kiume. Aidha, kikundi hiki cha maofisa wanafunzi ni cha 61 kutunukiwa kamisheni tangu utawala wa awamu ya kwanza wa Rais Mwl. Nyerere
-ARUSHA: Mkuu wa Majeshi, CDF Mabeyo amewaonya baadhi ya wanajeshi wanaojihusiha na mambo ya mitandaoni, akiwataka waache tabia hiyo mara moja.
-ARUSHA: Rais Magufuli ametangaza ajira kwa wanajeshi wapya 3,000 watakaoajiriwa na serikali hivi karibuni. Amesema atazingatia waliohitimu vyema mafunzo ya JKT.