






SHULE ya Sekondari St. Joseph ya jijini Dar es Salaam leo Septemba 23, 2017 imewakutanisha wanafunzi waliowahi kuosoma na kuhitimu kwenye shule hiyo na marafiki wengine katika kujenga umoja na mshikamano wa mawazo mbalimbali.
Hafla hiyo ya St. Joseph’s Alumni Day imefanika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar na kuhudhuriwa na wasomi wengi waliowahi kusoma shule hiyo.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo akiwa ni miongoni mwa waalikwa wa hafla hiyo, amehidhuria na kupata fursa ya kubadilishana mawazo na wanafunzi hao huku akiwapa mbinu tofauti za kukabiliana na changamoto za maisha ikiwa ni pamoja na mbinu za kufanikiwa katika ujasiriamali.
PICHA NA DENIS MTIMA | GPL