×

Polisi Wamwachia Peter Msigwa Usiku

Msigwa akishushwa kwenye gari la polisi.

MBUNGE wa Iringa Mjini (Chadema) Msigwa ameachiwa huru jana usiku  kwa dhamana baada ya kukamatwa akiwa kwenye mkutano wa hadhara.

Msigwa ameachiwabaada ya kudhaminiwa na wadhamini wawili Alex Kimbe pamoja na Mwenyekiti wa Bavicha Iringa  Leonce Marto , saa nne usiku .

Msigwa alishushwa  jukwaani kwa nguvu  akiwa anahutubia mkutano wa hadhara katika kata ya Mlandege Manispaa ya Iringa na anatuhumiwa kwa kosa la uchochezi dhidi ya vyombo vya usalama.

Tundu Lissu Kaanza Kazi Rasmi, Awahutubia Mawakili, Amuwakia Waziri Ummy

Marto  amesema  mikutano yake imefungiwa na hapaswi kuendelea na ziara yake katika kata nyingine  mpaka hapo OCD atakapo amua vinginevyo.

Leo  Mbunge anatakiwa kuripoti kwa RCO na huenda kesi ya uchochezi ambayo tayari imeshafunguliwa jalada lake ikapelekwa mahakamani .

Amesema  Mbunge huyo  atazungumza na vyombo vya habari leo mchana  kuweka wazi madhila yaliyompata wakati akitekeleza wajibu wake kwa wananchi.

Rais Magufuli: Tulipiga Marufuku Viroba kwa Sababu ya Maandamano ya Kisiasa

Leave a Comment