×

Washindi Sita wa M-Bet Wajichotea Milioni 195/=

m-bet
Msemaji wa M-Bet, David Malley, akizungumza mbele ya waandishi wa habari wakati wa kuwatangaza washindi.
m-bet
  Washindi wakikabidhiwa hundi zao.
m-bet
Mmoja wa washindi wa Milioni 26/=, Nchelu Leonce wa Geita, akizungumzia ushindi wake.

JUMLA ya washindi sita wa mchezo wa kubahatisha wameshinda kitita cha Sh milioni 26.7 kila mmoja baada ya kufanikiwa kubashiri timu 12 (Perfect 12)  katika bahati nasibu ya kampuni ya M-Bet.

 

Washidi hao ni  Satale Sandi kutoka Singida, Nelson Mlay (Moshi), Nchelu Leonce (Geita), Elia Malila (Katavi), Francis John (Arusha) na Enos Moshi wa Ifakara, Morogoro.

 

Akizungumza wakati makabidhiano leo, msemaji wa kampuni ya M-Bet, David Malley, alisema kuwa washindi hao wamebahatika baada ya kufanikiwa kubahatisha kwa usahihi  droo ya ‘Perfect 12 na kujiongezea kipato katika maisha yao.

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

Malley alisema kuwa droo hiyo inafanyika kila siku na kuwaomba wapenzi wa michezo ya kubashiriri kushiriki ili kujiongezea kipato.

 

Alifafanua kuwa washindi hao walitakiwa kupata sh milioni 32.5, lakini kutokana na kukatwa kodi asilimia 18, walipata kiasi hicho cha fedha ambacho si haba.

 

“Tunaomba Watanzania kucheza mchezo huu ili uweze kupambana na hali yako kama ilivyo kaulimbiu yetu. Michezo yetu ni ya uhakika na tunaamini kila mshiriki atajishindia kipato kikubwa,” alisema Malley.

 

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa hundi zao, Leonce alisema kuwa amefarijika na ushindi huo kwani ni faraja kwamba amecheza zaidi ya mwaka mmoja ili kupata mafanikio hayo.

 

“Nimefarijika sana, marafiki zangu walinikatisha tamaa ya kutocheza mchezo huu, sikuacha na leo nimefanikiwa kupata fedha, nitaongeza mtaji katika biashara zangu,” alisema Leonce.

Leonce pia aliiomba serikali kupunguza kodi katika fedha za washindi kufikia asilimia 10 kwani kwa sasa asilimia 18 inawaumiza.

 

 

Leave a Comment