
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri nchini huku akizigawanya baadhi ya wizara zikiwemo Wizara ya Kilimo na Mifugo, Nishati na Madini na kuongeza wizara mpya mbili na kufikisha jumla ya wizara 21. Katika Mabadiliko hayo, Mawaziri wawili na manaibu waziri wameongezwa.
Aidha Rais Magufuli ametangaza mabadiliko na kuteua Katibu mpya wa Bunge huku akieleza kuwa aliyekuwa Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila atapangiwa kazi nyingine.
ORODHA.
Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu: Naibu Waziri – Stella Alex Ikupa
Wizara ya Mifugo na Uvuvi: Waziri – Luhaga Mpina, Naibu Waziri -Abdallah Hamisi Ulega.
Wizara ya Maji na Umwagiliaj: Waziri- Mhandisi Isack Kamwelwe, Naibu Waziri – Jumaa Hamidu Aweso.
Wizara ya Nishati: Waziri – Dk. Medard Kalemani, Naibu Waziri – Subira Khamis Mgalu.
Wizara ya Madini: Waziri – Angellah Kairuki, Naibu Waziri -Stanslaus Haroon Nyongo.
Wizara ya Maliasili na Utalii: Waziri – Hamis Kigwanhalla, Naibu Waziri – Japhet Ngailonga Hasunga.
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji: Waziri –Viwanda/biashara – Dkt. Charles Mwijage, Naibu Waziri – Mhandisi Stella Manyanya.
Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia : Waziri – Prof. Joyce Ndalichako, Naibu Waziri -William Ole Nasha.
Wizara ya Fedha na Mipango: Waiziri – Dr Philip Mpango, Naibu Waziri – Dr Ashatu Kijaji.
