







WAHITIMU wa darasa la saba wa Shule ya Msingi ya St. Mary’s iliyoko Mbezi-Goigi, jijini Dar es |Salaam, jana walifanya mahafali ambayo yalifana na kuwavutia watu waliohudhuria hapo.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Shule hiyo Dkt. Rose Rwakatare aliwashukuru wazazi wa watoto hao kwa ushirikiano wao wa kuhakikisha wanafanikisha ndoto zao kwa kuwapatia elimu iliyo bora na akawaomba pia watoto hao mwakani wajiunge katika shule hiyo kwa masomo ya sekondari.
NA DENIS MTIMA/GPL