×

Kesi ya Lulu Yaunguruma, Mdogo wa Kanumba Asimulia Ugomvi Siku ya Tukio – (Pichaz + Video)

Lulu akiwa mahakamni.

KESI inayomkabili mwigizaji maarufu wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuhusishwa na kifo cha aliyekuwa staa wa filamu nchini, Steven Kanumba imeanza kuunguruma tena leo Alhamisi, Oktoba 19 katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

..Akiwa na mama yake mahakamni.

Katika kesi hiyo inayosikilizwa mbele ya Jaji Sam Rumanyika, ushahidi upande wa Jamhuri ulitolewa na mdogo wa marehemu Kanumba, Seth Bosco,  ambaye alikuwa shahidi wa kwanza.

Mama Lulu na Mama Kanumba wakitoka nje ya mahakama hiyo.

Akijibu swali la wakili wa utetezi, Peter Kibatala, shahidi Seth ameieleza mahakama hiyo juu ya ugomvi alioushuhudia kati ya Elizabeth Michael na marehemu Steven Kanumba siku ya tukio.

 

Familia ya Lulu wakijadili jambo na wakili Kibatala.

Seth  ameieleza mahakama kwamba anachofahamu yeye ni kuwa palikuwa na mgogoro kati ya Lulu na Kanumba aliousikia, uliosababishwa na simu kwamba, Lulu alikuwa akiongea kwa simu na mwanaume mwingine hali iliyozua ugomvi huo.

 

Mama Kanumba na familia yake wakifuatilia kesi hiyo.

Mbali na Seth, shahidi wa pili aliku,,wa ni daktari ambaye hata hivyo hakufika mahakamani hapo kwa kuwa aliomba udhuru kwa madai kuwa anaumwa. Jaji Rumanyika ameiahirisha kesi hiyo hadi kesho saa tatu. Mashahidi waliobaki ambao ni watatu watatoa ushahidi wao.

..Akizungumza jambo na mama yake.

Baadhi ya watu waliofika kusikiliza kesi hiyo ni mama mzazi wa Lulu, Lucresia Karugila, mama mzazi wa Kanumba, Flora Mtegoa, muigizaji Dkt. Cheni na wengine.

Lulu anakabiliwa na kesi ya kusababisha kifo cha Kanumba bila kukusudia, mnamo Aprili 7, 2012 .

VIDEO YA TUKIO HILO

Leave a Comment