×

Hakuna wa Kuyatabiri Maisha ya Mainda

MKONGWE kutoka kiwanda cha sinema za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amesema kuwa, hapa duniani hakuna ambaye anaweza kuyatabiri maisha yake yajayo isipokuwa Mungu pekee.

Mainda aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu kuwatabiria wenzao maisha yao kama vile wao ndiyo waliowaumba, jambo ambalo siyo sahihi.

“Sipendi kabisa mtu anitabirie maisha yangu…ooh…huyu yupo hivi, mara hivi, mara amefilisika, jambo ambalo ni baya sana katika maisha yetu ya kila siku maana ni Mungu pekee ndiye anayepanga maisha yetu,” alisema Mainda.

Stori: IMELDA MTEMA

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

Leave a Comment