TANZANIA kwa sasa inatafunwa na janga kuu linalohatarisha uhai wa ustawi wa jamii mithili ya virusi vinavyoua mwili! Janga hili limesababisha msiba mzito miongoni mwa wanajamii. Si lingine bali ni ushoga, Ijumaa Wikienda linakuletea ripoti kamili.
USHOGA NI NINI?
Katika mantiki ya makala haya, ushoga unaozungumziwa ni ule wa mapenzi ya jinsi moja kati ya mwanaume na mwanaume na siyo ushoga wa mwanamke na mwanamke ambao humaanisha urafiki wa kushibana.
UCHUNGUZI WA IJUMAA WIKIENDA
Katika mfululizo wa makala haya ya kushamiri kwa tatizo la ushoga nchini Tanzania, tutakuletea ripoti ya uchunguzi wa Gazeti la Ijumaa Wikienda, msimamo wa viongozi wakuu wa nchi kuanzia Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’, mawaziri, viongozi wa dini mbili kuu nchini; Waislam na Wakristo, viongozi wa kijamii, wataalam wa saikolojia, madaktari na watu wengine wa kada mbalimbali.
Uchunguzi huo wa gazeti hili ulijikita kujua tatizo linavyoanza,
yaani chanzo, linavyokua, kushamiri na madhara yake kwa jamii.
MMOMONYOKO WA MAADILI
Kwa jumla yake, kila aliyefikiwa na Ijumaa Wikienda alizunguka mulemule kwamba, kwa sasa jamii ya Kitanzania inakabiliwa na kasi ya mmomonyoko wa maadili ambayo husaidia kustawisha jamii ya ushoga.
Mengine yanayoambatanishwa na hilo ni usagaji, ukahaba, yaani biashara haramu ya ngono, uhusiano haramu wa kijinsia kabla ya ndoa na nje ya ndoa, kusambaa kwa sinema na picha za ngono hivyo kusababisha ongezeko la maradhi ya zinaa na mwisho ni kifo.
Yapo mengine yanayotajwa kuchochea kama uuzaji na utumiaji wa vileo na dawa za kulevya miongoni mwa vijana na ugumu wa maisha au tamaa ya kupata fedha bila kufanya kazi.
DINI ZINAKATAZA, NI DHAMBI
Yote yaliyotajwa
hapo juu ni mambo mabaya yasiyokubalika kwenye jamii iliyostaarabika na karibia dini zote na vitabu vitakatifu vinayataja kuwa ni dhambi kubwa na ni chukizo kwa Muumba wa Mbingu na Nchi (Mola).
Uchunguzi huo ulibaini kuwa, mambo hayo ndiyo yamekuwa yakizishughulisha zaidi jamii huku baadhi ya watu wakitumia maneno ‘potelea mbali au liwalo na liwe au maisha yenyewe mafupi’ hivyo kutojali hatari kubwa itakayowapata.
TAKWIMU RASMI
Kwa mujibu wa tafiti rasmi zilizofanywa na mashirika mbalimbali juu ya kushamiri kwa ushoga, takwimu zinaonesha kuwa kila siku ipitayo kiwango cha hatari kinazidi kuongezeka.
Baadhi ya watu waliozungumza na gazeti hili katika uchunguzi wake walieleza kuwa yapo mambo mengine yanayochochea mbali na hayo tuliyoeleza hapo juu kama ifuatavyo;
MALEZI
Watu wengi waliungana na kukubaliana kwamba, kwa sasa kuna tatizo kubwa la malezi ambapo wengi wa mashoga hao hukiri kuwa jambo hilo walifundishwa na ndugu, jamaa, marafiki, wafanyakazi wa kiume wa majumbani au wageni waliokuwa wakifadhiliwa na familia husika.
“Chanzo cha…(anatajwa mwanamitindo maarufu nchini) kuwa shoga ni kwamba, kuna wazungu walikuja nyumbani kwao zamani wakati akiwa mdogo. Hao ndiyo waliomfundisha hivyo alivyokua akajikuta ameshatumbukia kwenye dhambi hiyo,” anasema mmoja wa mtu wa karibu wa mwanamitindo huyo na kuongeza:
TAMAA YA MAISHA MAZURI
“Wengine ninaowajua ni vijana ambao mwanzoni walikuwa watoto wazuri kabisa, lakini kutokana na tamaa ya kutaka maisha mazuri. Matokeo yake wakajikuta wakirubuniwa na watu wenye ‘vihela’ vyao na kujikuta wameshapata tatizo.
“Kuna rafiki yangu mwingine wa kiume, yeye alikuwa anapenda tu maisha ya kujiachia ufukweni (wa Bahari ya Hindi) na kwenye mahoteli makubwa ilihali hana fedha. Kilichofuata ni kujirahisha kwa wazungu na sasa huwezi kuamini ukimuona ni shoga kabisa.
“Lakini pia siku hizi ukitembelea baa nyingi jijini Dar hasa Kinondoni na Sinza utashangazwa na ongezeko kubwa la mashoga, tena siku hizi hawajifichi kama zamani!”
Usikose wiki ijayo ambapo tutatoa ripori ya dalili za ushoga ambazo ukiziona kwa mwanaume ujue ndiyo hivyo tena! Pia tutaeleza namna ambavyo watu maarufu au mastaa wanavyochochea ushoga. Usikose!
Stori: Waandishi Wetu, Dar.
Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers
Android Bofya ===> Google Play
iOS Bofya ===>Apple Store
