
UTAMU wa takwimu kwa mchezaji unatokana na anavyojituma kusaidia jambo fulani hasa unapokuwa kiungo timu yako inacheza vizuri na kushinda au mshambulizi unayefunga mabao na kusaidia kuzalisha pointi.
Inawezekana pia ukawa mlinzi au kipa na kusaidia timu kutofungwa au kufungwa mabao machache. Zote hizi zinaingia katika takwimu.
Wachezaji wawili, Ibrahim Ajibu wa Yanga na Emmanuel Okwi ndiyo wanachochea watu 23,000 wanaoweza kuingia kwenye Uwanja wa Uhuru, wajikute wanashawishika zaidi kufanya hivyo.
Simba itakuwa inaivaa Yanga kwenye uwanja huo Jumamosi lakini gumzo limekuwa hao wawili na wanachotarajiwa kukifanya.
Yanga walikosa matumaini, hawakuwa na mtu wa kuwatishia watani wao kwa kuwa Amissi Tambwe na Donald Ngoma wanasumbuliwa na majeraha wakati Obrey Chirwa ndiyo anaanza kurejea lakini walikuwa na hofu kubwa na Emmanuel Okwi, pia Shiza Kichuya.

Lakini sasa, wakati Chirwa anarejea huku kukiwa na matarajio ya kuwaona Ngoma na Tambwe, anayebeba matumaini ya mioyo yao ni Ajibu ambaye amejiunga na Yanga akitokea Simba.
Takwimu za ndani zinaonyesha Ajibu kweli ni bora na tangu atue Yanga ameachana na “utoto” na sasa anapiga kazi na kweli inaonekana na Simba wana hofu h a s a kukutana na “kijana” wao m a a n a a n a fanya kazi yake.
O k w i na Ajibu wanaweza wakawa hawafanani sana kiuchezaji lakini majibu ya takwimu zao kwa wanachokifanya yanawafanya waonekane ni wa aina moja na wanaowapeleka watu uwanjani au kuwafanya wakae wakiangalia runinga.
Swali, Okwi au Ajibu watafanya nini, nani atafanya vizuri zaidi au yupi ataanza kufunga?
Kwa kasi w a l i y o n a y o wana nafasi ya kufanya vizuri kwa kufunga au kutengeneza nafasi ya kufunga. Lakini watatakiwa kutulia na kuwekeza akili zao, la sivyo mpira utawashinda kutokana na presha kubwa kuangushiwa vifuani mwao.
TAKWIMU ZAO:
MABAO:
OKWI:
Okwi ana mabao nane, matatu zaidi ya Ajibu akiwa amecheza dakika pungufu na hii inamfanya awe hatari zaidi kwa maana ya kuwa ana uwezo mkubwa zaidi wa kufunga licha ya kucheza dakika chache.
Okwi amecheza dakika 493 na Ajibu amecheza dakika 610.
AJIBU:
Ajibu ana mabao matano, lakini ameonyesha ni mwiba kwa kuwa mabao yake mengi hautarajii. Ni mchezaji ambaye atawapa wakati mgumu kumkaba na kwa kuwa angetaka kutimiza furaha yake kuifunga Simba, basi ataongeza juhudi na umakini.
UHURU:
OKWI:
Uwanja wa Uhuru ni kama nyumbani kuliko Ajibu kwa kuwa amefunga mabao yote nane katika uwanja huo. Inamp a n a f a s i y a kujiamini zaidi.
AJIBU:
Ajibu amefunga kwenye uwanja huo likiwemo bao zuri dhidi ya Ndanda FC. Lakini hiyo haimzuii kufunga au haimpi uhakika wa kufunga.
Ukiachana na bao lake dhidi ya Ndanda kwenye uwanja huo, Ajibu amefunga mabao dhidi ya Kagera Sugar-Kaitaba, dhidi ya Stand United akapiga mawili pale Kambarage.
Lakini kumbuka alifunga bao la mkwaju wa adhabu Yanga ikiwa ugenini dhidi ya Njombe Mji.
KICHWA:
OKWI:
Amefunga mabao mawili ya kichwa, hii i n amf a n y a kuwa na nafasi kubwa zaidi ya k u f u n g a k a m a Simba watatumia mipira ya krosi ingawa wana wapiga vichwa wazuri kama Kelvin Yondani na Nadir Haroub au Andrew Vincent.
AJIBU:
Hajafunga bao lolote la kichwa zaidi ya kuonyesha mguu wake wa kulia ni hatari sana. Kama haujajua, Ajibu ana uwezo mkubwa wa kupiga mashuti akipata nafasi na mfano ni bao lake la pili dhidi ya Stand.
KUJENGA:
OKWI:
Wanasema nafasi zinatengenezwa lakini unaweza kuzijenga vizuri kupitia timu au mtu. Okwi ana uwezo wa kutengeneza nafasi akiwa anakimbia na mpira na mkimuachia nafasi anaachia mkwaju na kufunga, katika mabao nane aliyofunga, mawili amefanya hivyo.
AJIBU:
Ajibu hakimbii sana na mpira, tofauti yake na Okwi anaweza kuwapita mabeki akiwa katika kasi. Ajibu ana uwezo wa kumuacha beki wakiwa wamesimama, akatoa pasi na kuchukua nafasi, yaani ni mzuri wa kutafuta nafasi na anaweza kuiboresha na mara nyingi hufanya hivyo wakati anapokea mpira.
Pasi aliyopewa na Chirwa katika mechi dhidi ya Stand, mpira alikuwa kama ameutuliza lakini tayari alishauinua kidogo kumpa nafasi ya kupiga shuti analotaka lakini alishampoteza beki aliyekuwa karibu yake.
FAULO:
Okwi na Ajibu wote ni hatari sana wanapokuwa nje na ndani ya eneo la 18, ni rahisi sana k u s a b a b i sha faulo kwa kuwa ni wepesi na si waoga kupita katikati ya msimu wa mabeki.
Mabeki wa kila upande wanapaswa kuwa makini na kama watajisahau kwa kusababisha faulo, pia ni kuwatengenezea nafasi.