×

Joti Alivyomvalisha Pete Mkewe Tumaini (Pichaz+Video)

Muigizaji wa vichekesho nchini kutoka Kundi la Orijino Komedi, Lucas Mhuvile ‘Joti’ akivishwa pete ya ndoa na mkewe wake  Tumaini Hassan katika Kanisa Katoliki la Magomeni leo jijini Dar.
Joti akijiandaa kumvalisha pete mkewe Tumaini.
…Joti akimvalisha pete mke.
…Wakipongezana baada ya kuvalishana pete za ndoa huku Joti akiongea jambo.

…Wakisonga mbele ya madhabahu kabla ya kuvalishana pete.
…Wakikumbatiana baada ya kuwa mke na mume baada ya kuvalishana pete.
…Wakiwa katika picha ya pamoja.

MUIGIZAJI wa vichekesho nchini kutoka Kundi la Orijino Komedi, Lucas Mhuvile ‘Joti’ ameuaga ukapela baada ya kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu, Tumaini Hasssan ndoa hiyo imefungwa Agosti 28, mwaka huu katika Kanisa Katoliki la Magomeni jijini Dar.

KIVUTIO

Kivutio kikubwa katika ndoa ya Joti na Tumaini ambao wamekaa kwenye uchumba kwa muda mrefu ni ile kumbukumbu ya kufanya tangazo la kufunga ndoa kwenye kampuni ya simu ya mkononi, Tigo ambapo leo wamefanya kweli jambo lililowavutia wadau na wapenzi wengi wa masuala ya burudani.

MSHANGAO

Mshhangao mkubwa katika ndoa hiyo ni kitendo cha bwana harusi Joti kuingia kanisani akiwa amenyoa mtindo unaojulikana kwa jina maarufu la kiduku ambapo wahudhuriaji wengi walionekana kushangazwa sana na jambo hilo lakini kwa upande wa Joti hakuonekana kujali hata kidogo na badala yake kuonesha fuaraha ya wazi kwa kitendo cha kufanikisha ndoa hiyo.

Sherehe ya kukata na shoka inatarajiwa kufanyika jioni ya leo ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, jinini Dar ambako watu wengi maarufu wanatazamiwa kuhudhuria.

PICHA: DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

Leave a Comment