×

Zitto Aijibu Tena Serikali ya JPM Kuhusu Takwimu za Pato la Taifa – Video

KIONGOZI Mkuu wa ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amefunguka tena akiituhumu serikali kupika twakwimu kuhusu kuongezeka kwa pato lataifa na kukua kwa uchumi wa nchi. Akizungumza na wanahabari katika Ofisi za makao makuu ya chama hicho, Zitto amesema Oktoba 20, 2017, Kamati ya Uongozi ya ACT Wazalendo ilifanya kikao Dar kujadili hali ya kisiasa na kiuchumi ya nchi na kutaarifiwa juu ya shaka ya kitakwimu za Ukuaji wa Pato la Taifa zilizotolewa BoT kati ya Aprili – Juni 2017. “Pato la Taifa la Tanzania lilisinyaa (contraction) kati ya Aprili na Juni mwaka 2017 tofauti na taarifa ya Serikali ilivyoeleza. Tumetumia taarifa za takwimu za Serikali kuchambua hali halisi, hatuvunji Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2015. Shaka iliyokuwapo juu ya kupikwa kwa takwimu za ukuaji wa Pato la taifa (GDP) ni halali, ni ya kweli na sasa tuna ushahidi. Taarifa ya mwisho ya Mapato ya Serikali iliyotolewa na TRA ni ya kupikwa haina uhalisia,” alisema Zitto. Hivi karibuni, Rais John Magufuli alitoa onyo kwa wanasiasa na wanaharakati wanaowapotosha wananchi kuwa pato la taifa limeshuka na kuwahadaa wananchi kuwa serikali imekua ikitoa taarifa zisizo za kweli kuhusu kukua kwa uchumi wa nchi ambapo Rais alisisitiza kuwapato la taifa limeongezeka ikilinganishwa na mwaka jana. Zitto amesema haya; “Nafahamu uchumi una lugha isiyo rafiki kwa walio wengi lakini nitajitahidi kutumia maneno rahisi ili wote tuelewane. Pato la Taifa (GDP) ni jumla ya mapato ya watu wote waliopo katika nchi au taifa husika katika kipindi maalumu,hususani mwaka mmoja. GDP ni kipimo cha uhai wa Uchumi wa Taifa,kwani ukuaji au uporomokaji wake hutumika kupima shughuli za kiuchumi za Taifa husika.

“Ukisikia GDP ni (+) maana yake kuna shughuli za uchumi zimeongezeka, Na (-) maana yake ni kuwa shughuli za uchumi zimepungua. Tanzania, tuna utaratibu wa kutoa takwimu za GDP kila baada ya miezi mitatu ambapo huita robo, mwaka mmoja una robo nne.

“Tafiti zinaonyesha kuwa, ili kuondoa umasikini wa Tanzania, uchumi wetu unatakiwa ukue zaidi ya 10% kwa miaka kama mitano mfululizo. Uchumi wa Tanzania haujawahi kukua kufikia 10% wakati wa utawala wote wa CCM. Kwa muda sasa, wastani wa ukuaji umekua ni 7%.

“Thamani ya bidhaa zilizouzwa kwenye nchi nzima hupatikana Kwa kuzidisha wastani wa bei na mzunguko wa bidhaa (transactions). Nchini Tanzania katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, mzunguko wa fedha umekuwa ni kati ya asilimia 0.5 na asilimia 1.5

“Je Pato la Taifa kwa mwaka 2015 na 2016 lilikuaje? Wananchi wanalalamika “Vyuma vimekaza. Ni wajibu wa mchumi kujiuliza inakuwaje tuna GDP inayokua wakati wananchi wanalia? Takwimu za makusanyo ya kodi za serikali kutoka TRA zinaacha mashaka makubwa mno kwani ni takwimu za kutengenezwa. Baada ya maelezo haya, mtakubaliana nami kuwa takwimu za Pato la Taifa Kwa robo inayoishia Juni 2017 si takwimu sahihi. ZIMEPIKWA! alisema Zitto.
 

 

Aidha Rais Magufuli alisema hivi karibuni kuwa, watu wanaopotosha umma kwa kupinga takwimu za serikali inapaswa ifike wakati wawe wanapelekwa mahakamani kuthibitisha kauli zao.

 
 

Leave a Comment