×

Mlipuko Waua Wanafunzi Sita Kagera

 

 

Wanafunzi sita wa Shule ya Msingi Kihinga mkoani Kagera, wamefariki dunia na wengine zaidi ya 40 wamejeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu wakicheza.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Augustine Orom amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari wananchi wamejitokeza kuchangia damu kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi.

Kwa mujibu wa Dokta Mariagoreth Fredrick ambaye ni Mganga Mkuu Hosipitali ya Rurenge, amethibitisha kupokea miili hiyo na majeruhi ambao baadhi wako katika hali mbaya na tayari wanapatiwa matibabu.

“Tulionao hali yao sio nzuri. Wengine wameumia matumbo, wengine wamechanika bandama, wengine wamevunjika miguu, wengine vichwa vimepata majeraha, wengine wameumia macho,” alisema Dokta Mariagoreth wakati akizungumza na BBC.

Inaelezwa kwamba kabla ya kulipukiwa na kifaa hicho kinachodhaniwa kuwa ni bomu, wanafunzi hao walikuwa wanakichezea.

Leave a Comment