×

Wauza Mbolea Bila Leseni Kufikishwa Mahakamani

Mkaguzi wa mbolea Mariki akizungumza na mfanyabiashara wa bidhaa hiyo.
Mariki akiendeleza oparesheni
Mariki akikagua mbolea.

DAR ES SALAAM: MAMLAKA ya Udhibiti Mbolea Tanzania (TFRA), leo, Alhamis, Novemba 9, 2017, imetinga katika Soko Kuu la Kariakoo jijini hapa na kukagua leseni pamoja na bei elekezi kwenye maduka ya wafanyabiashara wa mbolea katika soko hilo.

 

Katika ukaguzi huo ulioongozwa na Alan Mariki, mkaguzi wa mbolea kutoka TFRA na kufanyika majira ya saa tano za asubuhi, ulibaini wamiliki wengi wa maduka hayo ya mbolea hawana leseni jambo ambalo ni kinyume na sheria.

 

Akizungumza na Global TV Online, Mariki alisema kuwa kwa wauzaji wa Kariakoo hasa kwenye soko hilo wamekwisha pewa semina zaidi ya mara moja, juu ya bei elekezi ambapo ni shilingi 36, 584, lakini pia umuhimu wa kumiliki leseni za biashara hiyo, pamoja na upatikanaji wake.

“Hawa wafanyabiashara ambao hawana leseni wanakiuka sheria na kiukweli wanafanya kiburi katika hili, sasa sisi tutawapeleka mahakamani ili wawajibishwe kwa mujibu wa sheria,” alisema Mariki.

 

Global TV Online iliweza kuzungumza pia na baadhi ya wafanyabiashara hao wa mbolea, ambapo kwa upande wa Edna Lyimo alisema kuwa ni ukweli kwamba wamekwisha pewa semina juu ya umuhimu wa leseni na yeye alikuwa kwenye hatua za kukamilisha jambo hilo.

 

“Kiukweli tumekwisha pewa elimu juu ya hili, binafsi ni matatizo tu yaliyojitokeza kwenye familia yangu maana mwanangu aliungua na maziwa, lakini katika siku mbili hizi nilikuwa ninafanya ‘process’ za kupata leseni na kabla ya kupata ndiyo hivyo tena tumekuja kukamatwa,” alisema Edna.

 

Aidha Edna, alilalamikia juu ya bei elekezi na kudai kwamba hazipo wazi kiasi cha kufanya wafanyabiashara hao kuzifahamu, na kuomba mamlaka husika kutazama namna ya kuziweka wazi!

Leave a Comment