×

WANNE MAHAKAMANI KWA KUMZOMEA MKE WA RAIS MUGABE!

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe

Watu Wanne wamefikishwa mahakamani nchini Zimbabwe kwa kosa la kumzomea mke wa rais wa nchi hiyo, Robert Mugabe, Bi Grace Mugabe.

Kwa mujibu wa gazeti la serikali la nchi hiyo, watu hao wameshtakiwa kwakosa la kudharau mamlaka ya rais.

Mke wa Rais wa Zimbabwe, Grace Mugabe

Mahakama ilipata taarifa kuwa siku ya Jumamosi, watu hao waliimba nyimbo na kuonyesha ishara katika mkutano wa hadhara wa chama tawala {ZANUPF}.

Na Isri Mohamed

Leave a Comment