×

Video: Mama Kanumba Aishukuru Mahakama Kumhukumu Lulu

Mama wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa,  akiongea na wanahabari nje ya Mahakama Kuu leo, ametoa pongezi kwa mahakama hiyo kwa kutenda haki katika kumhukumu mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwenda jela miaka miwili kwa kumuua bila kukusudia aliyekuwa mwigizaji mwenzake, Steven Kanumba.

Aliongeza kwamba hukumu hiyo itamfanya marehemu mwanaye alale vyema zaidi kaburini mwake ambako mama huyo alisema angekwenda mara moja kulitembelea.

Leave a Comment