×

Simba Yawafunga Tanzania Prisons Bao 1-0 Uwanja wa Sokoine Mbeya

Kikosi cha timu ya Tanzania Prisons.

SUB -Hamisi Maingo anaingia kuchukua nafasi ya Kimenya

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 90 Prisons wanaonekana kutokata tamaa, wanaendelea kupambana kupata bao la kusawazisha
Dk 89 Kipa Prisons analazimika kutoka na kuokoa mbele ya Bocco
Dk 87 Manula yuko chini pale, inaonekana amegongana na Mwasote
Dk 86, Kimenya anaachia mkwaju mzuri hapa inakuwa goal kick
GOOOOOOOOOOOOOO Dk 84 Bocco alikuwa kama anaanguka, anageuka na kupiga shuti kali kabisa na kuandika bao

Mshambuliaji wa Simba, John Bocco (katika) akifanya yake.

SUB Dk 78, Ally Shomari anaingia kuchukua nafasi ya Muzamiru Yassin
Dk 77 krosi nzuri ndani ya lango la Prisons lakini Bocco na Mavugo wanaukosa mpira

Dk 75, Prisons wanapata kona yao ya tatu baada ya Kotei kugongeshwa lakini Sabianka, anapiga kona dhaifu
Dk 74 mpira wa adhabu wa Erasto Nyoni, unatoka juu kidogo ya lango la Prisons, goal kick
Dk 72, Prisons wanamuweka chini Mo Ibrahim

SUB Dk 60 Niyonzima anakwenda benchi, nafasi yake inachukuliwa na Mohamed Ibrahim
Dk 60 krosi nzuri ya Niyonzima, Prisons wanaokoa vizuri kabisa

Dk 55 Prisons wanafanya shambulizi kubwa zaidi, Simba wanaokoa na kuwa kona, inachongwa na Kimenya, Simba wanaokoa

Dk 52, Manula analazimika kutoka nje ya lango lake na kuokoa, unakuwa wa kurushwa
Dk 48, Kichuya anajaribu akiwa nje ya 18 likiwa shuti lake la kwanza, goal kick
Dk 47 mpira mzuri wa Niyonzima, Bocco anaingia lakini Chona yuko vizuri, goal kick

Dk 45, Prisons wameanza kwa kasi wakionekana wamepania kupata bao la mapema

MAPUMZIKO
-Eliuta anamtoka Kotei anakwenda chini, anaachia mkwaju lakini kipa Manula anadaka vizuri kabisa

MAPUMZIKO

-Eliuta anamtoka Kotei anakwenda chini, anaachia mkwaju lakini kipa Manula anadaka vizuri kabisa

ZIMEONGEZWA DK 2

Dk 44, Kimenya anamkanyaga Kotei hapa, mwamuzi anamuonyesha wakati wachezaji wa Simba wakilalamika

Dk 42, mpira unaendelea kubaki eneo la katikati mwa uwanja kwa dakika tatu sasa

Dk 39 mpira umesimama kuna mchezaji wa Prisons yuko chini pale

Dk 38 sasa, mpira unaonekana kubaki katikati ya uwanja zaidi

Dk 30 sasa, kila timu inaonekana kujilinda zaidi na kufanya mashambukizi ya kushitukizaDk 27,krosi ya Niyonzima, Bocco anaweka ndani lakini Mpalile anaokoa mpira ukiwa unavuka mstari

Dk 25, Mlipili anafanya kazi ya ziada kuokoa krosi ya Kimenya na kuwa kona, inachongwa vizuri, Simba wanaokoa

Dk 23, Simba wanagongeana vizuri lakini Kazimoto anachelewa na mwamuzi anasema ni goal kick

Dk 21, Rashid anaingia vizuri lakini mwamuzi anapuliza kipyenga, anasema amefanya madhambi kwa kumsukuma Kotei

Dk 18 Kassim wa Prisons naye anajaribu vizuri kwa kuachia shuti, goal kick

Dk 16, Bocco anawaacha mabeki wa Prisons lakini shuti lake nyanya kabisa

Dk 10, Kichuya anaachia mkwaju mkali kabisa naye hakulenga lango

Dk 7, Mohamed Rashid anaingia vizuri lakini shuti lake halikulenga lango

Dk 1, Prisons ndiyo wanaanza kwa kasi lakini wanaonekana hawako mapema

Aishi Manula

Erasto Nyoni

Mohamed Hussen “Tshabalala”

James Kotei

Yusuph Mlipili

Jonas Mkude

Shiza Kichuya

Mzamiru Yassin

John Bocco

Mwinyi Kazimoto

Haruna Niyonzima

Sub;

Emanuel Mseja

Ally shomary

Nicholas Gyan

Laudit Mavugo

Juma Liuzio

Mohamed Ibrahim “MO”

PICHA: MUSA MATEJA | GLOBAL PUBLISHERS

Leave a Comment