SEHEMU ya jengo la kituo cha Clouds Media Group lililoko Mikocheni jijini Dar es Salaam limeungua moto jana ambapo Mkurugenzi wa Vipindi wa kituo hicho, Ruge Mutahaba, amesema moto huo ulitokea bila ya mtu yeyote kuwa na taarifa nao ambapo ulianzia katika studio ndogo ya kurekodia.