
DAR ES SALAAM: Wakati Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akionyesha nia yake ya kuikomesha biashara ya uchangudoa ndani ya himaya yake, maswali yameibuka kama anajua uwepo wa hoteli na gesti kugeuzwa madanguro.
Awali, kwa kiasi flani Makonda alifanikiwa kudhibiti wadada hao waliokuwa wakijipanga barabarani, lakini kwa sasa inaonekana wadada hao wameibuka kwa kasi na mbinu mpya ya kujiuza kwa kujipanga nje ya gesti au hoteli kwa kujiuza mchana na usiku huku wakiwa wamepanga katika vyumba vya hoteli au gesti husika.
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini baadhi ya gesti na hoteli katika maeneo mbalimbali ya Sinza ambazo zimegeuzwa madanguro kwa kuwafuga mabinti hao ambapo moja ya danguro hilo lilinaswa maeneo ya Sinza Mori jijini Dar ambalo hufanya shughuli hiyo saa 24 za siku.

Danguro hilo ambalo kwa nje lina kibao kinachoonyesha ni nyumba ya kulala wageni (Gusasa), linawahusisha wasichana wadogo kiumri na wasichana wa kati, ambao huifanya kazi hiyo kuanzia asubuhi hadi jioni kwa malipo ya bei chee kabisa. Hili liligundulika baada ya hapo awali, Kitengo Maalum Cha Operesheni Fichua Maovu (OFM) kupewa ubuyu wa kuwepo kwa danguro hilo.
Chanzo chetu kilisema licha ya kuandikwa kibao cha kuonyesha kuwa ni nyumba ya kulala wageni, lakini mtu hawezi kupata chumba hapo kwa muda wote wa siku, kwani wasichana hao wamevikodi vyote na wanavilipia. OFM ilipofika eneo hilo na kujiridhisha, iliamua kuingia kazini na kubisha mlango kwa ajili ya kuhitaji chumba yako siyataki tena (baada ya kuzungumza kwa ukali, anaondoka akiwa amekasirika huku akimmwagia matusi makali kamanda wa OFM).
Vibinti vilivyokutwa katika nyumba hiyo, ambavyo huonekana vikirandaranda eneo hilo kunasa wateja, wanakadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 17-18 huku baadhi ya madadapoa hao, wakiaminika kuwa ni wake za watu.

Inadaiwa kuwa wanawake hao huaga majumbani mwao kuwa wanafanya kazi katika baadhi ya viwanda vidogovidogo vilivyoko maeneo mbalimbali Mwenge, lakini huishia katika nyumba hiyo na kufanya uchangudoa wao.
Jirani mmoja na eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina la Kawesh, alisema siyo wanawake wote wanaojiuza hapo hulala, kwani baadhi yao huondoka jioni na kurejea asubuhi, wakati wapo ambao huingia jioni na kuondoka asubuhi. “Biashara ya ngono hapa ni muda wote, ni kama wanapeana shifti hivi.

Maana kuna wadada unawaona mchana tu, usiku hawapo, na wengine wanaonekana usiku tu, mchana huwaoni, halafu hata mwenye nyumba hii hatumfahamu, nadhani serikali ingefanya wepesi kuliondoa danguro hili kwani litawaharibu vijana wetu,” alisema. Juhudi za Amani kumfahamu mmiliki wa nyumba hiyo bado zinaendelea, lakini wakati huohuo linatoa wito kwa wahusika, hasa Polisi, kumsaidia mkuu wa mkoa katika kuliondoa tatizo la uchangudoa, ambalo limekuwa likiota mizizi kila siku,