×

David Kafulila Ajiunga Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole akimuapisha aliyekuwa mbunge wa zamani wa Jimbo la Kigoma Kusini (2010-2015), David Kafulila.

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amemuapisha aliyekuwa mbunge wa zamani wa Jimbo la Kigoma Kusini (2010-2015), David Kafulila alijivua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutokana na kutokuwa na imani na upinzani katika kupambana na ufisadi.

Kafulila aliwahi kuwa mwanachama wa NCCR-Mageuzi na kushinda nafasi ya ubungewa jimbo hilo na alikuwa ndiye mbunge aliyeongoza suala la utafunaji wa fedha za Escrow, fedha ambazo ziligawanywa kwa watu wa matabaka mbalimbali serikalini na maeneo mengine.

Katika uchaguzi uliopita, Kafulila aligombea tena ubunge lakini alishindwa na alipofungua kesi kupinga matokeo hayo bado alishindwa mahakamani. Hii hapa chini ndo barua yake.

Leave a Comment