×

Samia Suluhu Amwakilisha JPM Kuapishwa kwa Kenyatta

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo asubuhi tarehe 28 Novemba, 2017 amewasili Mjini Nairobi nchini Kenya ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba amepokelewa na Mhe. Balozi Robinson Njeru Githae wa Kenya na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. Pindi Chana.

Sherehe za kuapishwa kwa Mhe. Rais Uhuru Kenyatta zinafanyika katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Nairobi

28 Novemba, 2017.

=====

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akitia saini kitabu cha wageni baada ya kuwasili Nairobi, kumwakilisha Rais Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa Rais Uhuru kenyatta leo.

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

 

LIVE: Waziri Mkuu Azungumza na Waandishi wa Habari

Leave a Comment