




WAZIRI wa habari, Utamaduni sanaa na michezo, Dkt.Harison Mwakyembe amezindua kituo cha wasanii kitakachokuwa kikisambaza na kusimamia kazi za wasanii kiitwacho Barazani.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mwakyembe amesema kuwa lengo kubwa la kituo hicho litakuwa kusaidia wasanii kusambaza kazi zao kwa faida na kwa uwazi kupitia teknolojia ya mitandao.