Mwenyekiti UVCCM Taifa Apandishwa Kizimbani Akidaiwa Kugawa Rushwa
Global Publishers December 11, 2017
SHARE THIS:
Sadifa akiwa mahakamani leo.
DODOMA: Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Sadifa Juma Khamis (Mb.) amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma leo akishitakiwa kwa kosa la kutoa rushwa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo.
LIVE: Matokeo ya Uchaguzi UVCCM Taifa Yatangazwa- Dodoma
Sadifa ambaye alikamatwa na maofisa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) nyumbani kwake jana eneo la Mnada wa Zamani, Dodoma, akidaiwa kutoa rushwa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UVCCM, Taifa kutoka Mkoa wa Kagera kwa ajili ya mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika Dodoma amepandushwa kizimbani mjini humo leo Desemba 11, 2017 ili kujibu mashtaka hayo yanayomkabiri.
TAKUKURU ilimnasa akitoa hongo kwa wajumbe ikidaiwa kwa lengo la kumpitisha Mgombea Thobias Mwesiga.