×

Rais Dkt. Samia Aweka shada la maua katika kaburi la Chifu wa Wangoni (Picha +Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua katika kaburi la Chifu Msaidizi wa Wangoni Nduna Songea Mbano ambaye pia alinyongwa na kukatwa Kichwa na Wajerumani mwaka 1906.

Rais Dkt. Samia ameanza ziara ya kikazi mkoani Ruvuma ambapo atakagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi.

Rais Samia akiweka shada la maua katika Mnara wa Mashujaa Songea Mkoani Ruvuma.
Matukio mbalimbali wakati Rais Samia alipotembelea Makumbusho ya Vita vya Majimaji, Songea mkoani Ruvuma tarehe 23 Septemba, 2024.

 

Leave a Comment