×

Miili ya Wanajeshi 14 wa JWTZ Waliouawa DRC Yaagwa, Mmoja Wao Hajapatikana

MAMIA ya waombolezaji wamejoteka kuaga miili ya askari 14 waliouawa na waasi wa ADF nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambapo shughuli ya kuaga miili ya askari hao imefanyika leo Alhamisi, Desemba 14, 2017 katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Upanga jijini Dar es Salaam.

 

Katika shuguli hiyo ya kuaga, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameongoza waombolezaji Viongozi wengine waliohudhuria katika kuaga miili hiyo ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo, wakuu komandi za anga, maji, nchi kavu na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), viongozi wa Umoja wa Mataifa, na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, askari na wananchi.

 

Akizungumza wakati wa kuaga, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo amesema; “Jeshi la Wananchi linafanya uchunguzi wa kina, tukio hili ni kubwa na baya zaidi, lakini halitatuvunja moyo, linazidi kutuimarisha, na Tanzania haitarudi nyuma katika kutoa wanajeshi wetu kutumikia vikosi vya UN. Wanajeshi wengine 44 ambao ni majeruhi wa tukio hilo wanaendelea na matibabu katika miji ya Kampala, Kinshasa na Goma, huku askari mmoja akiwa bado hajapatikana,” alisema Mabeyo.

VIDEO: SHUHUDIA SHUGHULI YA KUAGA MIILI HIYO IKIFANYIKA